Wachezaji Wanaongoza kwa Asisti NBC 2024/2025
Utangulizi
Hapa tunaangazia Watoa Asisti Bora Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2024/2025, ambako tutashuhudia ubunifu na vipaji vinavyoleta burudani ya kipekee kwenye soka la Tanzania. Msimu huu, viungo na washambuliaji mahiri kutoka klabu mbalimbali kama Simba, Yanga, Azam FC, na zingine, wamejituma kutengeneza nafasi muhimu za mabao. Hapa, utapata takwimu, uchambuzi wa mbinu za baadhi ya wachezaji mahiri, na namna wanavyochangia mafanikio ya timu zao. Fuatilia hapa ili kujua ni nani anayebeba taji la mtaalamu wa kutoa asisti msimu huu wa 2024/2025.
Hadi sasa, Feisal Salum wa Azam na Pacome Zouzoua wa Young Africans wanaongoza kwa utoaji assist NBC msimu huu.
Wachezaji Wanaongoza kwa Asisti NBC 2024/2025
Hadi kufikia sasa, wachezaji 30 walio na idadi kubwa ya asisti ni hawa wafuatao:
# | Mchezaji | Timu | Utaifa | Asisti |
---|---|---|---|---|
1. | Feisal Salum | Azam | Tanzania | 12 |
2. | Pacome Zouzoua | Young Africans | Ivory Coast | 8 |
3. | Max Nzengeli | Young Africans | DR Congo | 7 |
4. | Ki Stephane Aziz | Young Africans | Burkina Faso | 7 |
5. | Jean Ahoua | Simba | Ivory Coast | 7 |
6. | Prince Dube | Young Africans | Zimbabwe | 7 |
7. | Josephat Bada | Singida BS | Ivory Coast | 7 |
8. | Salum Kihimbwa | Fountain Gate | Tanzania | 5 |
9. | Ismail Mgunda | Mashujaa | Tanzania | 4 |
10. | Mohamed Hussein | Simba | Tanzania | 4 |
11. | Heritier Makambo | Tabora UTD | DR Congo | 4 |
12. | Iddy Selemani | Azam | Tanzania | 4 |
13. | Elie Mpanzu | Simba | DR Congo | 4 |
14. | Ladaki Chasambi | Simba | Tanzania | 4 |
15. | Amosi Kadikilo | Fountain Gate | Tanzania | 3 |
16. | Salmin Hoza | Dodoma Jiji | Tanzania | 3 |
17. | Emmanuel Keyekeh | Singida BS | Ghana | 3 |
18. | Salehe Masoud | Pamba Jiji | Tanzania | 3 |
19. | Yacouba Songne | Tabora UTD | Burkina Faso | 3 |
20. | Marouf Tchakei | Singida BS | Togo | 3 |
21. | Shomari Kapombe | Simba | Tanzania | 3 |
22. | Leonel Ateba | Simba | Cameroon | 3 |
23. | Ande Koffi | Singida BS | Ivory Coast | 3 |
24. | Clement Mzize | Young Africans | Tanzania | 3 |
25. | Mudathir Yahya | Young Africans | Tanzania | 3 |
26. | Banele JR Sikhondze | Tabora UTD | Eswatini | 3 |
27. | Redemtus Mussa | KMC | Tanzania | 3 |
28. | Datius Peter | Kagera Sugar | Tanzania | 3 |
29. | Kibu Denis | Simba | Tanzania | 3 |
30. | Pius Buswita | Namungo | Tanzania | 2 |
Uchambuzi wa Asisti kwa Baadhi ya Wachezaji
Feisal Salum (Azam 2024/25)
Feisal ameendelea kung'ara katika safu ya kati ya Azam, akitoa pasi mahiri zinazowarahisishia washambuliaji kufunga mabao. Uwezo wake wa kusoma mchezo na kutengeneza nafasi za hatari unamfanya kuwa kiungo muhimu kwa Azam msimu huu.
Salum Kihimbwa (Fountain Gate 2024/25)
Kihimbwa, akiwa mshambuliaji matata, amekuwa akichangia asisti muhimu ambazo zinaboresha uimara wa safu ya ushambuliaji ya Fountain Gate. Kasi yake na ushirikiano mzuri na viungo wa timu vinachangia mabao mengi zaidi.
Jean Ahoua (Simba 2024/25)
Ahoua, kiungo tegemeo wa Simba, ameonyesha kiwango kizuri katika kutoa pasi za mwisho. Mbinu zake za kukokota mpira na uwezo wa kusambaza mipira kwa usahihi unamfanya awe tegemeo la kutengeneza nafasi za mabao.
Ki Stephane Aziz (Young Africans 2024/25)
Aziz ameonyesha uwezo wa kupenya safu za ulinzi za wapinzani, akitengeneza nafasi murua kwa washambuliaji. Ubunifu wake katika kuchezesha timu na kutoa pasi zenye macho kumemfanya kuwa lulu muhimu ndani ya Young Africans.
Ismail Mgunda (Mashujaa 2024/25)
Mgunda ni mshambuliaji mwenye mbinu na kasi, anayesaidia siyo tu kufunga, bali pia kutoa asisti zinazowapa mabao wachezaji wenzake. Ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Mashujaa wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo ndani ya muda mfupi.
Pacome Zouzoua (Young Africans 2024/25)
Zouzoua ameonyesha ubunifu mkubwa anapokuwa na mpira, akitawanya pasi za kuvunja ulinzi wa wapinzani. Uelewano wake na wachezaji wengine wa Young Africans unazalisha fursa nyingi za mabao, hivyo kumfanya awe mmoja wa watoa asisti bora msimu huu.
Maswali kwako Shabiki wa NBC
- Ni mchezaji gani unayemwona ataongoza kwa asisti hadi mwisho wa msimu huu?
- Je, unafikiri kuna mchezaji ambaye hajatajwa lakini ana uwezo wa kuibuka na kuwa mtoa asisti bora?
Angalia Pia
-
Mega Odds za Leo | Acca Tips
Angalia mega odds za leo. Acca Tips zenye nafasi kubwa ya ushindi le...
-
Mikeka ya Over 1.5
Angalia mikeka yetu ya leo ya Over 1.5 na mbinu za kushinda mikeka hii...
-
Mikeka ya Over 2.5
Angalia mikeka yetu ya leo ya Over 2.5 na mbinu za kushinda mikeka hii...
-
Mikeka ya Over 0.5 First Half
Angalia mikeka yetu ya leo ya Over 0.5 kipindi cha kwanza, ligi nzuri na mbinu za kushinda mikeka hii...
-
Sure 3 | Betslip ya Siku
Angalia Odds 3 za uhakika leo. Hii hapa betslip ya siku yenye odds za uhakika 3 leo...
-
Mikeka ya Over/Under 3.5
Angalia mikeka yetu ya leo ya Over/Under 3.5, ligi na mbinu za kushinda mikeka hii
-
Mikeka ya Correct Score
Pata mikeka ya correct score kila siku bure. Mikeka ya uhakika ya correct score leo na kesho
-
Kampuni Bora za Betting Tanzania
Angalia list ya kampuni bora 5 za betting Tanzania kwa mwaka huu...
-
Mbinu za Kushinda Betting
Jifunze mbinu za kushinda betting zako na uondokane na hasara za mara kwa mara...
-
Misimamo ya Ligi Kuu
Angalia misimamo ya ligi kuu mbalimbali duniani. Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Ratiba na Matokeo