Wafungaji Bora England Premier League 2024/2025. Je, Nani Atamaliza Msimu Kinara wa Magoli?

Updated on: Thursday, April 3, 2025 at 03:00 AM

Utangulizi

Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) 2024/2025 ni mojawapo wa msimu wa kusisimua wenye ushindani wa hali ya juu. Kama ilivyo kawaida, mabao ni sehemu muhimu ya mchezo, na kila shabiki anafuatilia kwa karibu orodha ya wafungaji bora ili kuona nani ataibuka kinara mwishoni mwa msimu. Katika chapisho hili, tunakuletea orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa mabao hadi hivi sasa pamoja na maoni na uchambuzi wa jinsi wanavyoweza kuendelea kufanya vyema.

Hadi sasa, Mohamed Salah wa Liverpool na E. Haaland wa Manchester City wanaongoza kwa mabao ndani ya ligi hii ya Uingereza yenye mchuano mkali sana.

Orodha ya Wafungaji Bora (Top Goal Scorers) EPL 2024/2025

Hadi hivi sasa, wachezaji hawa wameonyesha umahiri mkubwa wa kufumania nyavu. Hapa chini ni orodha ya wafungaji bora Ligi Kuu England:

# Mchezaji Timu Magoli Penati
1. Mohamed Salah Liverpool 27 9
2. E. Haaland Manchester City 21 2
3. A. Isak Newcastle 20 2
4. C. Wood Nottingham Forest 18 3
5. B. Mbeumo Brentford 16 5
6. Y. Wissa Brentford 14 0
7. C. Palmer Chelsea 14 3
8. Matheus Cunha Wolves 13 0
9. O. Watkins Aston Villa 13 2
10. J. Mateta Crystal Palace 12 2
11. J. Kluivert Bournemouth 12 6
12. L. Delap Ipswich 11 2
13. J. Strand Larsen Wolves 10 0
14. R. Jiménez Fulham 10 3
15. L. Díaz Liverpool 9 0
16. J. Maddison Tottenham 9 0
17. N. Jackson Chelsea 9 0
18. K. Havertz Arsenal 9 0
19. B. Johnson Tottenham 9 0
20. C. Gakpo Liverpool 8 0
Orodha hii inasasishwa mara kwa mara kulingana na mechi za kila wiki.
Ona pia, Orodha ya Watoa Asisti Bora wa EPL 2024/25



Je, Wachezaji Hawa Wanapata Vipi Mabao?

Erling Haaland (Manchester City)

Haaland amekuwa moto wa kuotea mbali, akitumia nguvu zake, kasi, na umakini wa hali ya juu kumalizia nafasi anazopata. Timu ya Manchester City ina mtindo wa uchezaji unaomfaa sana huyu mwamba, huku viungo wengine wakimlisha pasi zenye ubora mkubwa.

Mohamed Salah (Liverpool)

Salah ameendelea kuwa mchezaji tegemeo wa Liverpool, akitumia kasi na ufundi wake kuwatungua mabeki wa timu pinzani. Uwezo wake wa kufunga mabao kwa mguu wa kushoto unamfanya awe mshambuliaji wa kipekee ndani ya EPL.

Cole Palmer (Chelsea)

Kwa upande wa Palmer, licha ya kuwa kijana, ameonyesha ukomavu na uwezo wa kufunga mabao muhimu kwa Chelsea.

Kwa ujumla, ushindani wa mfungaji bora wa EPL msimu huu wa 2024/2025 unaonekana kuwa mkali, na utakuwa wa kusisimua kuona nani ataibuka kidedea mwishoni mwa msimu.